Lava Lava Ng’ari Ng’ari Lyrics
(Ayolazer)
(Dopabeat)
Nimetulizana ndege kwa kiota sitoki Mambo mwororo
Nimenasiana hata kwa kuku kutwa sing’oki
Kwa minyororo
Nishasahau zamani kushikana mashati mizozo
Mapenzi gani kila kukicha vibonzo
Nimepata mwandani bila VAT bila tozo
Wambea kunani mnakipi kina mama nyonzo
Na nimeamua sitaki sitaki
Kurudia matapishi nishakula yamini divai
Aende akanishitaki mahakamani polisi
Kama kuna kitu ananidai
Ooh poleni wanokonoko
Penzi linameta meta meta
Mwali fundi si kitoto
Kama kasomea veta veta
Mwiteni na kiroboto
Mje na matarumbetambeta
Sisi twachochea moto
Roho kuwakereketa
Penzi linang’ara, ng’ari ng’ari
Mtaliona hivi hivi, ng’ari ng’ari
Kwa mbali linapepea, ng’ari ng’ari
Mtaliona ivi ivi, ng’ari ng’ari
Wenyewe twajifaidia
Aniita, aniitani ayuni
Namwita nyonda sabuni
Anipa anipa mpaka mafuli
Sio mbwembwe ndio zake tamaduni
Najua mimi niko peke yangu
Ndo maana natamba
Sina shaka hofu kwa raha zangu
Hata mkinichamba
Wenye roho za kwanini
Nitajijua zangu niko naye sambamba
Mi napenda yake anapenda yangu
Kuilamba lamba
Zifikisheni salamu kwa yule kidudu mtu
Mwambie kutesa kwa zamu asipige marufuku
Yaani ni mashamu shamu leo mambo iko huku
Nimepata bekamu fundi si butubutu
Ooh poleni wanokonoko
Penzi linameta meta meta
Mwali fundi si kitoto
Kama kasomea veta veta
Mwiteni na kiroboto
Mje na matarumbetambeta
Sisi twachochea moto
Roho kuwakereketa
Penzi linang’ara, ng’ari ng’ari
Mtaliona hivi hivi, ng’ari ng’ari
Kwa mbali linapepea, ng’ari ng’ari
Mtaliona ivi ivi, ng’ari ng’ari
Wenyewe twajifaidia
Mwenzenu napewa vitamu, tende halua halua
Vya pwani vya bara, tende halua halua
Anipa haninyimi wala, tende halua halua
Mwenzenu nalishwa nalala, tende halua halua
Aah
Wasafiii